Mahusiano ya Stevo Simple Boy na Mrembo Jenny Wangui yamefika mwisho ikiwa ni miezi miwili tangu wawili hao waanze kuchumbiana.
Stevo amefuta picha zote akiwa na mrembo huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram siku chache baada ya watumiaji wa mtandao wa Tinder kuibua madai kuwa Jenny Wangui ana akaunti kwenye mtandao huo wa kuwatafuta wapenzi.
Utakumbuka jana Jenny Wangui aliibuka na kudai kuwa hakuwahi toka kimapenzi na mkali huyo wa Ngoma ya “Freshi Barida” kwa kuwa mahusiano yao yalikuwa ya kuigiza kwa ajili ya kuutangaza muziki wa Stevo Simple Boy.