You are currently viewing PENZI LA TANASHA DONNA NA OMAH LAY  LAKOLEA MITANDAONI

PENZI LA TANASHA DONNA NA OMAH LAY LAKOLEA MITANDAONI

Moja kati ya headlines zinazo gonga vichwa vya habari mtandaoni ni issue inayomtaja mwanamuziki wa Nigeria Omah Lay kutoka kimapenzi na staa wa muziki nchini Tanasha Donna, sakata ambalo kila mtu analizungumzia katika namna yake.

Katika nyakati tofauti tofauti kwa pamoja kupitia insta story zao kwenye mtandao wa Instagram Wawili hao wameshare picha zinazo onekana kushabihiana eneo moja ikiwemo hoteli wanaodaiwa kuwa wamekuwa wakijivinjari huko Mombasa huku wote wakipost kwenye muda unao tofautiana dakika moja tu.

Vyanzo vya karibu na Tanasha, vinadai Hitmaker huyo wa “Gere” na Omah Lay wamekuwa pamoja mjini Mombasa tangu msanii huyo atue nchini Kenya jambo linalodaiwa kuwa lilimpelekea Omah Lay kususia kutumbuiza katika tamasha la Beach Fest  kwenye mkesha wa kuamkia mwaka mpya kutokana na kulewa na penzi la Tanasha Donna.

Tetesi za Tanasha na Omah Lay kuwa kwenye mahusiano zilianza mwaka jana walipoonekana pamoja nchini Nigeria na Sudan Kusini wakiwa wanakula bata pamoja lakini pia walikuwa wakiachia comment za mahaba kwenye picha zao kwenye mtandao wa instagram jambo liliwaaminisha mashabiki kuna kitu kinaendelea kati yao.

Hata hivyo hakuna mmoja kati yao amejitokeza kuthibitisha kama kweli wapo kwenye mahusiano ila ni jambo la kusubiriwa maana waswahili wana msemo wao unaosema penzi ni kikozi na halifichiki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke