You are currently viewing PENZI LA WEEZDOM NA MYLEE STACY LAFUFUKA TENA, WAOMBANA MSAMAHA HADHARANI

PENZI LA WEEZDOM NA MYLEE STACY LAFUFUKA TENA, WAOMBANA MSAMAHA HADHARANI

Aliyekuwa msanii wa nyimbo za Injili nchini Weezdom ameamua kumuomba msamaha mpenzi wake wa zamani Mylee Stacy ikiwa ni siku chache zimepita tangu amporomoshee mvua ya matusi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Weezdom amekiri kumvunjia heshima mpenzi wake wa zamani Mylee Stacy ambaye kwa mujibu wake wamepitia changamoto nyingi kimaisha kwa kusema kwamba anajutia kitendo cha kumdhalilisha hadharini kwenye mitandao ya kijamii.

Msanii huyo ametumia fursa hiyo pia kuwaomba msamaha wanawake wote wote ambao amekuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi na kuahidi kuwa atawapa heshimu kwa mchango wao kwenye safari yake ya maisha .

Hata hivyo Ex wake Mylee Stacy alishuka kwenye uwanja wa comment ya post yake na kuachia ujumbe wa kukubali msamaha wake, jambo lilozua mjadala mzito miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya Kijamii ambao walionekana kushangazwa na hatua ya Weezdom kurudiana na Ex wake Mylee Stacy, wengi wakihoji huenda wawili hao wamekuwa wakipanga matukio ya kuchafuana mtandaoni ili waweze kuzungumziwa kwenye  majukwaa ya burudani nchini.

Ikumbukwe kauli ya Weezdom imekuja siku chache baada ya paparazi mmoja kuvujisha mtandaoni video yake akiwa na Mylee Stacy ambapo walionekana wakielekea nyumbani kwa Weezdom.

 

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke