Msanii wa Sailors Gang Peter Miracle Baby kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu tuhuma zilizokuwa zikimuanda za kuwatelekeza wanawake aliozaa nao.
Katika mahojiano na Mungai Eve, Miracle Baby amekanusha madai ya kuwa na wanawake wengi kwa kusema kwamba wanawake wote waliokuwa wanadai amepata nao watoto kwenye mitandao ya kijamii walikuwa wanatumia jina lake kujitafutia umaarufu mtandaoni.
Katika hatua nyingine amewajibu walimwengu waliokuwa wanadai kuwa amekaliwa sana na mke wake Carol Katrue kwa kusema kwamba madai hayo hayana msingi wowote kwa kuwa ni mapenzi ya dhati aliyonayo kwa mke wake ndio yamewafanya watu kuanza kumzungumzia vibaya.
Utakumbuka kipindi cha nyuma wanawake mbali mbali walijitokeza mtandaoni wakidai kwamba wana ujazito wa Peter Miracle Baby jambo ambalo lilipelekea mke wake Carol Katrue kurushiana maneno makali na baadhi ya wanawake hao kama njia ya kumkingia kifua mume wake.