Kiungo wa kimataifa wa Brazil na Barcelona Philippe Coutinho atajiunga na Aston villa Kwa mkopo hadi, mwisho wa msimu.
Vilabu vya Aston Villa na Barcelona vimekubaliana juu ya uhamisho wa nyota huyo na villa watalazamika kulipa sehemu ya mshahara wake.
Inatajwa kuwa Kiungo huyo ameshawishika zaidi kujiunga na Villa kutokana na Meneja wa Klabu hiyo Steven Gerrard kwa sababu walicheza wote Liverpool.
Kiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 29 aliichezea Klabu ya Liverpool kwa miaka mitano (2013-18) kisha kujiunga na Barca ambayo aliitumikia kwenye michezo 76 kisha kutolewa kwa mkopo katika Klabu ya Bayern Munich na sasa Aston Villa.