You are currently viewing PIA PONDS AFUNGUKA UGOMVI WAKE NA REMA NAMAKULA

PIA PONDS AFUNGUKA UGOMVI WAKE NA REMA NAMAKULA

Pia Pounds alisainiwa na Eddy Kenzo chini ya lebo yake ya muziki ya Big Talent  wakati Mshindi huyo wa Tuzo ya BET alikuwa akichumbiana na Rema Namakula.

Wakati wanandoa hao walitengana mwaka wa 2018, baadhi ya mashabiki wa muziki nchini Uganda walidai kwamba Pia ponds ndio chanzo cha wawili hao kutengana.

Ingawa amekuwa akikataa kuzungumza juu ya Rema Namakula, katika mahojiano ya hivi karibuni, Pia Pounds amedokeza kuwa yeye na Rema Namakula sio marafiki na huwa hawazungumzi.

“Siongei na Rema Namakula kwa sababu sisi sio marafiki. Ni hayo tu, sitaki kuzungumza zaidi juu yake, “amesema Pia Ponds.

Hata hivyo, hitmaker huyo wa “Tupaate” amekataa kuweka wazi kwa nini hawazungumzi na Rema Namakula.

Ikumbukwe Pia Pounds na Eddy Kenzo kwa sasa ni marafiki kwani miezi kadhaa iliyopita waliachia wimbo wa pamoja uitwao “Tuupate Remix” wakiwa na MC Africa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke