You are currently viewing Pia Ponds akiri kutumia pesa zote za akiba kwenye surgery ya jino

Pia Ponds akiri kutumia pesa zote za akiba kwenye surgery ya jino

Msaniii wa kike kutoka nchini Uganda Pia Ponds amekiri kutumia pesa zake za akiba kwenye shughuli ya kupata jino jipya baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya ya barabarani.

Kwenye mahojiano yake hivi karibu Mrembo huyo amesema mchakato wa upasuaji wa kupata jino jipya nchini Kenya ulimgharimu pesa nyingi kiasi cha kutumia mirahaba ya wimbo wake Tupaate kufanikisha matibabu yake.

Hitmaker huyo “sSlay Farmers” ambaye amekuwa akificha sana kwa umma amewataka mashabiki kukaa mkao wa kupokea ujio wake mpya ambao utakuwa wakitofauti kama alivyozoeleka kwenye muziki wake.

Pia Ponds sio msanii wa kwanza kuweka maneno ya bandia nchini Uganda, kipindi cha nyuma tuliona msanii wa Swangz Avenue Azawi akifanya hivyo alipopata umaarufu kupitia wimbo wake wa “Quinamino”

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke