You are currently viewing PIA PONDS AWAACHA MASHABIKI NJIA PANDA KUHUSU MWAANDISHI WA HITSONG YAKE “TUPAATE”

PIA PONDS AWAACHA MASHABIKI NJIA PANDA KUHUSU MWAANDISHI WA HITSONG YAKE “TUPAATE”

Female singer kutoka nchini Uganda Pia Ponds amewaacha mashabiki na maswali mengi kuhusu ni nani hasa alimuandikia wimbo wake wa “Tupaate”.

Hii ni baada ya mrembo huyo kuibuka na kujinasibu kuwa yeye ndiye mwaandishi halisi wa wimbo huo kauli ambayo inakinzana na aliyoitoa mwaka wa 2021 aliposema kuwa msanii mwenzake Azawi ndiye alihusika kwenye uandishi wa ngoma hiyo ambayo inapatikana kwenye EP yake mwaka wa 2020 “Tupaate”.

Mrembo huyo alienda mbali zaidi na kujinasibu kuwa yeye ni moja kati ya waandishi wazuri wa nyimbo wenye vipaji nchini Uganda.

Utakumbuka wimbo wa “Tupaate” kutoka kwa Pia Ponds uliachia katikati mwaka mwa 2020 lakini ilikuja ikapata umaarufu Afrika Mashariki wakati video ya Mc Africa akiwa anavibe na wimbo huo iliposambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Ilikuwa ni mshangao kwa Pia Ponds kupata hitsong kwenye safari yake muziki ikizingatiwa kuwa wakosoaji wa muziki wake wamekuwa wakidai kuwa hana kabisa cha kuimba.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke