You are currently viewing Picha ya Messi yavunja rekodi Instagram

Picha ya Messi yavunja rekodi Instagram

Baada ya nguli wa mpira wa miguu Lionel Messi kushinda Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia ya kucheza mpira wa miguu, historia nyingine mpya imewekwa huko Instagram.

Nyota huyo wa soka wa Argentina alichapisha picha zake akiwa ameshikilia Kombe la Dunia kwenye ukurasa wake wa Instagram, chapisho ambalo kwa sasa linashika rekodi ya chapisho lililopendwa zaidi ‘most liked Instagram post’.

Katika muda wa saa 48 tangu lichapishwe, lilikuwa na ‘likes’ milioni 62 na hadi sasa lina zaidi ya likes milioni 68.2.

Kabla ya picha ya Messi kuchukua rekodi hiyo, picha iliyokuwa ikishika nafasi hiyo tangu 2019 ni picha ya yai ambayo ndiyo picha pekee kwenye akaunti ya World Record Egg

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke