You are currently viewing PILIPILI AFUNGUKA KUHUSU UKIMYA WAKE KWENYE MUZIKI

PILIPILI AFUNGUKA KUHUSU UKIMYA WAKE KWENYE MUZIKI

Mwanamuziki mkongwe nchini Pilipili amefunguka sababu za ukimya wake kwenye muziki.

Akizungumza na KOM, Pili pili amesema hajaacha muziki kama inavyoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii ila alichukua mapumziko mafupi kwa ajili ya kujipanga vizuri kimuziki baada ya kuachia nyimbo kali.

Licha ya ukimya wake kwenye game ya muziki, msanii huyo amesema bado anafanya matamasha ya muziki na haijawahi pita hata mwezi mmoja bila ya yeye kutumbuiza kwenye shows.

Hata hivyo amesema hajakuwa akiachia nyimbo kwenye mainstream media kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wake ila kwa sasa anajipanga na timu yake ya mauzo kabla hajarejea rasmi kwenye muziki.

Pilipili ni moja kati ya wasanii walioacha alama kwenye muziki mapema miaka ya 2000 kwa kuachia hits kali kama Mpaka Che, Kamata Dem,Morale na nyingine kibao lakini alikuja akapotea kwenye game ghafla huku akiwaacha mashabiki na maswali mengi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke