Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Pitson na mkewe wake Caroline Nyokabi wametangaza kuwa wanatarajia kumpata mtoto wao wa tatu hivi karibuni.
Pitson ameweka wazi taarifa hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake Instagram alipochapisha picha akiwa na mke wake ambaye ni mja mzito na kusindikiza na caption inayosomeka “Tangazo, tangazo!, Praise God with us”
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Lingala ya Yesu” tayari amebarikiwa kuwapata watoto wawili pamoja na mke wake Caroline Muthoni ambao Havilah Geitherer na Taji.
Pitson anakuwa msanii wa hivi punde kujiunga kwenye orodha ya mastaa ambao tayari wametangaza kuwa wanatarajia kupata watoto hivi karibuni