Staa wa muziki kutoka Marekani Post Malone amewaondolea hofu mashabiki wake kuhusu afya yake baada ya kupata ajali mbaya akiwa jukwaani kwenye moja ya onesho lake huko St. Louis.
Mkali huyo wa ngoma ya “Rockstar” ametoa taarifa kwa mashabiki kwamba anaendelea vizuri huku akiomba radhi kwa kuwaeleza kuwa atarejea tena St. Louis wakati mwingine kwa ajili ya show.
Lakini pia amesema ziara yake “Twelve Carat Tour” itaendelea kama kawaida.
Utakumbuka wikiendi hil iliyomalizika, Show ya Post Malone haikuisha vizuri katika ukumbi wa Enterprise Center mjini St. Louis kufuatia mkali huyo kuanguka jukwaani na kuumiza mbavu zake tatu.
Post Malone alitumbukia kwenye shimo ambalo lilikuwa pembezoni mwa jukwaa ambapo timu ya madaktari ilifika eneo hilo ambalo Post Malone alikuwa akilia kwa uchungu na kumpa huduma ya kwanza kabla ya kukimbizwa hospitalini kwa matibabu zaidi.