Mrembo wa Nigeria, Precious Okoye ameshinda taji la Urembo la Afrika (Miss Africa) mwaka 2022.
Okoye mwenye miaka 27 ameibuka mshindi katika shindano ambalo limefanyika usiku wa kuamkia leo ambapo warembo 20 wamepanda jukwaani kuwania taji hilo.
Kwa matokeo hayo, Okoye anakuwa Mnigeria wa kwanza kushinda taji hilo la urembo la Afrika.