You are currently viewing PREZZO AIDHINISHWA NA IEBC KUWANIA UBUNGE

PREZZO AIDHINISHWA NA IEBC KUWANIA UBUNGE

Rapper aliyegeukia siasa Jackson Ngechu maarufu Prezzo ameshindwa kuficha furaha yake baada ya tume ya IEBC kumuidhinisha kuwa atawania ubunge wa eneo la Kasarani kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9 kupitia Tiketi ya chama cha Mabadiliko Na Busara.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Prezzo amethibitisha taarifa hiyo kwa kusema kwamba amekithi vigezo vyote ambavyo tume ya IEBC ilikuwa inahitaji kutoka wagombea huru ya kuwasilisha saini 1,000 huku akidokeza mpango kuanza kuomba uungwaji mkono kutoka kwa wananchi.

“The Revolution Shall Be Televised! IEBC Requirements For An Independent Ticket Was 1000 Signatures. Iam Happy To Say That We Surpassed That & Now It’s Time To Hit The Grounds. Chama Madiliko Na Busara! #CMB #PrezzoForKasarani #NgwareNaMapema“, ameandika Instagram.

Prezzo anaungana na Wasanii wengine walioidhinishwa na IEBC kama Bahati anayewania ubunge Mathare kupitia Tiketi ya Jubilee, mchekeshaji Jalang’o ambaye ni mgombea wa ubunge Lang’at kupitia cha cha ODM, Gabu anayewania Mwakilishi Wadi ya Woodley Golf Course kupitia Chama cha AMANI na MC Jessy ambaye ni mgombea wa ubunge, Imenti Kusini.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke