Rapper Prezzo, Sanaipei tande na Mchekeshaji maarufu nchini ambaye pia ni mgombea wa ubunge langat Jalang’o wametajwa kuwa miongoni mwa mastaa 10 na wachekeshaji 17 wa kenya ambao watarajiwa kushirikishwa kwenye show mpya ya ucheshi iitwayo Roast House.
Show hiyo inalenga kusherekea mafanikio na machango wa mastaa mbali mbali nchini Kenya kupitia ucheshi ambao utafanywa na kundi la wachekeshaji wa majukwaani.
Roast House ina maonyesho au Episodes 10 za dakika 24 kila moja ambayo itawapa nafasi kwa wachekeshaji kutoa burudani na vichekesho wakiangazia madai, kauli mbiu na matukio mbali mbali maishani kwa ajili mastaa watakao kuwa wamealikwa.
Roast House ambayo itaruka hewani Julai 14 mwaka huu imetayarishwa na eugene mbugua kwa ushirikiano na D & R studios pamoja na makundi ya wachekeshaji kutoka nchini Kenya.