You are currently viewing PRINCE INDAH ASITISHA TOUR YAKE MAREKANI KISA CORONA

PRINCE INDAH ASITISHA TOUR YAKE MAREKANI KISA CORONA

Mwanamuziki kutoka Kenya Prince Indah amesitisha ghafla ziara yake ya kimuziki nchini Marekani mara baada ya kukutwa na kirusi cha corona pamoja na mmoja wa wanachama bendi yake.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Prince Indah amethibitisha taarifa hiyo kwa masikitiko kusema kwamba wamesitisha safari zote hadi pale watakapotoa tarehe nyingine ya kuendelea na ziara hiyo.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Girwa Ni” ameomba radhi mashabiki zake wa nchini Marekani waliokuwa wamenunua mtandaoni tiketi za kuhudhuria shoo zake huku akiwataka wamuweka katika maombi ili aweze kupata nafuu ya kuendeleza ziara yake ya muziki.

“We remain strong to fight our battle till the end, our faith in He who is in heaven is unshaken forever and ever. It is with much pain in my heart to announce that our travelling to the U.S.A have been cancelled due to Covid+ cases that was earlier detected from one member of my crew and myself. This forced our travelling be postponed to a later date …

To our American fans and more so who had booked their tickets online, we are sincerely sorry for the inconvenience caused by this; we pray for better result so that we reschedule our dates soon.” Ameandika Facebook

Hata hivyo mashabiki zake wamesikitishwa na taarifa hiyo mbaya ambapo wamemtumia salama za kumtakia afueni ya haraka pamoja mwanachama wa bendi yake ya malaika Band.

“ Too unfortunate , pole sana Malaika Band, we do trust your service when Music is a concern just soon we resume enjoying the very best of you. Much love!!” , “It shall be well prince…quick recovery.”  Mashabiki wameandika

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke