Ex wa msanii Stivo Simple Boy, Pritty Vishy amezua gumzo mtandaoni baada ya kukiri hadharani kuwa atahudhuria harusi ya mkali huyo wa ngoma ya Freshi Barida.
Katika kikao cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram vishy amesema anaogopa makalio yake yaatamchanganya kimawazo Stivo kwenye siku yake hiyo muhimu.
Sanjari na hilo amesema haoni ndoa ya Stivo na mpenzi wake Gee ikidumu kwa kuwa anajua uyonge wa msanii huyo linapokuja suala la unyumba.
Hata hivyo amemtolea uvivu msanii huyo wa Men in Business kutokana na suti aliyokuwa amevaa juzi kati kwa kusema kwamba mtindo wa suti hiyo ni wa kizamani sana, hivyo waliomvalisha walifeli kinoma.
Utakumbuka Vishy ambaye anaidaiwa kutoka kimapenzi na msanii Madini Classic alikuwa kwenye mahusiano na Stivo Simple Boy lakini walikuja wakaachana kutokana na madai ya usaliti.