You are currently viewing PRITTY VISHY ALIZWA NA KITENDO CHA ADASA KUTAKA KUMUIBIA MPENZI WAKE MSANII STIVO THE SIMPLE BOY

PRITTY VISHY ALIZWA NA KITENDO CHA ADASA KUTAKA KUMUIBIA MPENZI WAKE MSANII STIVO THE SIMPLE BOY

Mpenzi wa mwanamuziki Stivo The Simple, Pritty Vishy ameonekana kukerwa na kitendo cha msanii Adasa kuonekana kumzimia kimahaba rapa huyo kwenye moja ya video aliyoshare kwenye mtandao wa Instagram.

Kwenye video hiyo ambayo wapo ufukweni mwa bahari Hindi, Adasa anaonekana akipiga stori na Stivo the Simple wakiwa matembezini ambapo ghafla aliaanza kumzungushia kiuno akiwa katika pozi la kimahaba zaidi, jambo ambalo lilimfanya Pritty Vishy ashuke kwenye uwanja wa comment ya post hiyo na kumpa Adasa somo akae mbali na mpenzi wake Stivo The Simple Boy, la sivyo atamfunza adabu.

Hata hivyo Adasa alishindwa kumvumilia vitisho vilivyotolewa na mrembo huyo ambapo nae aliamua kujibu mapigo kwa kujitapa kwamba wakati Pritty Vishy kuwa na Stivo The Simple Boy kimahusiano ulishaisha kitambo, hivyo ni zamu yake kumuonesha msanii huyo mapenzi mujarab.

Sasa baada ya kutunishiana misuli kwenye mtandao wa Instagram Prityy Vishy aliamua kwenda live instagram akiwa mwenye huzuni huku akiilaani vikali   kitendo cha Stivo the simple boy kumsaliti kimapenzi kwa kutoka na Adasa ambaye kwa mujibu amzidi na chochote.

Hata hivyo hatua ya wawili hao kurushiana maneno makali hadharani kisa mwanaume imeibua hisia miongoni mwa walimwengu kwenye mitandao ya kijamii ambao wamehoji kuwa huenda wawili hao wanajaribu kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa kabla ya ujio wa ngoma mpya ya Stivo The Simple aliyomshirikisha Adasa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke