Mchumba wa msanii Stivo The Simple Boy ametangaza kuachana na msanii huyo baada ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa muda.
Akipiga stori na mzuka kibao Pritty Vishy amesema amechukua maamuzi ya kuachana na Stivo the simple baada ya msanii huyo kuonekana kutomdhamini kwani amekuwa akiusikiliza sana uongozi wake wa Made In Kibera.
Kauli ya Pritty Vishy inakuja siku chache baada kudai kuwa uongozi wa Made in Kibera umekuwa ukimnyanyasa Stivo the Simple kwa kupora pesa zake ambazo amezitolea jasho kupitia muziki.
Hata hivyo Stivo The Simple hajatoa tamko lolote kuhusiana na madai ya Pritty Vishy ila ni jambo la kusubiriwa