Mchumba wa msanii Madini Classic, Pritty Vishy amezua gumzo mtandaoni mara baada ya kukiri hadharani kuwahi kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
Kupitia insta stori yake kwenye mtandao wa Instagram mrembo huyo amesema alikuwa anavutiwa kimapenzi na wanawake wenye makalio makubwa.
” Mi nishawahi, Ilikua dame tulikutana naye Facebook. Nlikuwa curious kujua lesbians hufanya nini. Si tukaslide mpaka Whatsapp. Akanituamia nudes zake na akaniambia nimgtumie zangu. na Nikatuma mpaka video.” alisema akijibu shabiki yake aliyetaka kufahamu kama amewahi kuvutiwa na wanawake wenzake kimapenzi.
Pritty vishy alipata umaarufu nchini baada ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii Stivo Simple Boy lakini walikuja wakaacha kwa madai ya usaliti.
Kwa sasa mrembo huyo yupo kwenye mahusiano mengine na msanii Madini Classic mahusiano ambayo yameanza kuyumba kutokana na wawili hao kutokuwa na ukaribu tofauti na walivyokuwa wanatambulisha mahusiano yao kwa umma.