You are currently viewing Pritty Vishy na Tiktoker Becky Akinyi wadaiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja

Pritty Vishy na Tiktoker Becky Akinyi wadaiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja

Mtengeneza maudhui nchini Kenya Pritty Vishy na Tiktoker Becky Akinyi wamewaacha mashabiki wakijiuliza maswali iwapo wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Hii ni baada ya video kusambaa mtandaoni ikimuonesha Pritty Vishy akimnyanyua Becky walipokuwa wakicheza muziki na kisha wakaendelea kupigana mabusu.

Lakini pia walichapisha video nyingine kwenye TikTok live wakiwa kwenye mahaba mazito kwenye mazingira ya klabu.

Mashabiki wao kwenye mtandao wa TikTok walitoa hisia tofauti huku wengi wakihoji kuwa huenda wawili hao wanaodai kuwa marafiki wa karibu wameanza kushiriki mapenzi ya jinsia moja.

Ikumbukwe miezi kadhaa iliyopita Pritty Vishy alionyesha nia ya kimapenzi kwa mwimbaji wa nyimbo za injili Daddy Owen baada ya mwimbaji huyo kufichua kwamba alikuwa anatafuta mke wa kuingia nae kwenye ndoa.

Mwanamuziki huyo hata hivyo alikataa ombi lake akidai kuwa foleni ya wanawake wanaotaka kimapenzi ilikuwa ndefu

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke