You are currently viewing PRODYUZA BONGA KUFANYA KAZI TENA NA HARMONIZE BAADA KUTOFAUTIANA KIMAWAZO

PRODYUZA BONGA KUFANYA KAZI TENA NA HARMONIZE BAADA KUTOFAUTIANA KIMAWAZO

Mtayarishaji wa muziki wa Bongofleva maarufu kama Prodyuza Bonga ambaye alihusika kukamilisha hit song ya ‘Never Give Up’ ya Harmonize ameeleza kufanya tena kazi na mwanamuziki huyo mmiliki wa record label ya Konde Gang baada ya kutofanya naye kazi kwa muda mrefu kufuatia kutofautiana.

Mtayarishaji huyo amefunguka hayo kupitia insta story yake kwenye mtandao wa instagram akijibu moja ya maswali ya mashabiki waliotaka kujua kama atafanya kazi tena na Konde Gang, na kujibu kuwa tayari zipo kazi nyingi sana.

Lakini pia kwenye post nyingine ameweka wazi kwamba atafanya kazi na Harmonize kwa makubaliano ya mkataba.

Mapema mwaka jana Prodyuza Bonga alitangaza kuacha kufanya kazi na msanii huyo kwa madai ya kutolipwa na kutotimiziwa baadhi ya ahadi ikiwemo kununuliwa gari baada ya wimbo wa “Never Give Up” kufanya vizuri.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke