Mtayarishi maarufu wa muziki nchini “Cedo” Kadenyi ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la “Ceduction.”
Ceduction album imebeba jumla ya mikwaju 16 ya moto huku zote zikiwa ni kolabo pekee.
Cedo ambaye amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa takriban miaka 20 amewashirikisha wasanii mbali mbali wa Afrika Mashariki kama Nyashinski, Khaligraph, Karun, Trio Mio, Arrow Boy, Naiboi, Rich Mavoko, Aslay, Rema Namakula, Lydia Jasmine na wengine wengi.
Album ya “Ceduction” ni album ya kwanza ya mtu mzima Cedo tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Boomplay,Spotify na Apple Music.