You are currently viewing Prodyuza Magix Enga azua gumzo mtandaoni baada ya kuonekana akiwa mlevi kupindukia

Prodyuza Magix Enga azua gumzo mtandaoni baada ya kuonekana akiwa mlevi kupindukia

Video ya mtayarishaji muziki nchini Kenya Magix enga akiwa katika hali mbaya imesambaa mitandaoni.

Katika video hiyo, prodyuza huyo anaonekana akiwa amekaa chini ya mti katika mavazi yaliyochanika huku akiwa mlevi.

Video ambayo awali ilisambaa kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa Tiktok ilizua taharuki mitandaoni, huku baadhi ya Wakenya wakiwataka wasamaria wema kumuokoa msanii huyo mwenye kipaji cha kipekee kutoka kwenye kadhia ya kubugia pombe kupindukia.

Awali, magix enga alifichua kwamba alilazimika kujiunga na kituo cha matibabu ya watumiaji wa madawa, pombe na mihadarati ili kumsaidia kukabiliana na uraibu wake wa pombe. Baadaye aliruhusiwa kwenda nyumbani na tangu wakati huo alianza kufanya kazi na wasanii tofauti kama kawaida wakiwemo wasanii wa boondocks gang.

Magix Enga ni miezi michache amegonga vichwa vya habari baada ya kukiri kwamba aliingia Illuminati kumbe ilikuwa kiki ya mziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke