Prodyuza maarufu wa muziki wa Gengetone nchini Mavo On The Beat ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la “Unajifanya.”
Unajifanya album imebeba jumla ya mikwaju 17 ya moto huku zote zikiwa ni kolabo pekee.
Mavo On The Beat ambaye amekuwa kwenye tasnia ya muziki kwa takriban miaka 10 amewashirikisha wasanii mbali mbali kama Wyre, Daddy Andre, Jua cali, Naiboi, Masauti, Exray, Mejja, Breeder LW, Rekless, Okello Max, Ssaru, Trio Mio na wengine wengi.
Album ya “”Unajifanya” ni album ya kwanza ya mtu mzima Mavo On The Beat tangu aanze safari yake ya muziki mwaka 2013 na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Boomplay,Spotify na Apple Music.