Mtayarishaji mkongwe kwenye muziki nchini Teddy B amejipata pabaya baada ya kukumbwa na tuhuma za kumtapeli msanii chipukizi aitwaye Shanki.
Kwa mujibu wa Shanki alimlipa prodyuza huyo kiasi cha Ksh 20,000 kwa ajili ya kumrekodia wimbo ila amekuwa akimkwepa toka mwezi Januari mwaka huu.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter amechapisha picha ya mazungumzo kati yake na Teddy B huku akisindikiza na ujumbe unaosomeka, “Huyu music Producer anaitwa Teddy B anakuaga mwizi mkubwa sana. Ukishamlipa anaku block na anakatalia project,”
Hata hivyo mpaka sasa Teddy B hajijibu juu ya tuhuma hizo ila ni jambo la kusubiriwa.