Prodyuza Totti amedhibitisha kumtema msanii Ally B kwenye label yake ya muziki ya wa KG Record kwa kile alichokitaja kuwa alikiuka makubaliano ya mkataba.
Totti amesema walizozana kwa sababu ya malipo ya shows pamoja utayarishi wa nyimbo za siasa za mwana siasa mmoja tajika kutoka kaunti ya Mombasa.
Totti amesema project iliyositishwa imempa hasara kubwa kwani alikuwa amewalipa baadhi ya waandishi wa nyimbo zilizo kuwa ndani ya Album ya Ally B.
Hata hivyo Ally B amepinga madai kuwa hakuwa muwazi kwa Totti kuhusu malipo ya shows na kusema kuwa walikubalina kusitisha kufanya kazi kwa pamoja.
Hitmaker huyo wa Maria amesema anaendelea kutayarisha Album yake na prodyuza tofauti kwa sababu idea ya nyimbo hizo zilikuwa ni zake.
Mapema mwaka huu Totti alitangaza kuwa Ally B amesaini mkatba na lebo yake ya KG records na walikuwa wana tayarisha album mpya, baada ya kufanya singo mbili ambazo ni Take You Home na Amapiano ya kimiji.