You are currently viewing PRODYUZA WA BONGOFLEVA NAHREEL AKANUSHA KUWA NA MTOTO NJE YA NDOA

PRODYUZA WA BONGOFLEVA NAHREEL AKANUSHA KUWA NA MTOTO NJE YA NDOA

Msanii wa muziki Bongofleva Nahreel amekanusha vikali taarifa za kuzaa nje ya mahusiano yake na mpenzi wake, Aika ambaye wanaunda wote kundi la Navy Kenzo.

Nahreel kupitia ukurasa wake wa Instagram ametaka wote wanaosambaza taarifa hizo kuiheshimu familia yake ambapo amesisitiza ana watoto wawili tu aliojaliwa na Aika.

“Kutokana na habari zinazosambaa kwenye blog mbalimbali na watu mbalimbali maarufu pia wamekuwa wakipost bila kuwa na ushahidi wowote, hizi habari sio za kweli.

“Nina watoto wawili, Gold na Jamaika, na nimezaa na mwanamke mmojaAika, kuweni makini mnapotoa habari familia yetu haiendekezi Umbeya ila hii imevuka mipaka.” Ameandika Nahreel kupitia Instagram page yake.

Utakumbuka Nahreel na Aika wako mbioni kuachia album yao mpya inayokwenda kwa jina la Dread & Love ambayo wamedai imekamilika kwa asilimia 70.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke