You are currently viewing PRODYUZA WA BONGOFLEVA YOGO BEATS ATANGAZA KUACHA MUZIKI

PRODYUZA WA BONGOFLEVA YOGO BEATS ATANGAZA KUACHA MUZIKI

Prodyuza wa muziki wa Bongofleva, Yogo Beats ametangaza kuacha muziki bila kueleza sababu hasa iliyomplekea kuchukua maamuzi hayo magumu.

Kupitia Instagram Yogo ameandika; I quit the game, staki tena muziki. f******** this game.

Mara baada ya ujumbe huo, Wasanii na Maprodyuza mbalimbali wamemsihii asifanye hivyo kwenye post aliyoichapisha kwenye mtandao wa instagram.

Hata hivyo, mtayarishaji mwenzake Mandugu Digital ame-comment kwa kuandika ujumbe unaosemeka “Mkitaka asiache milipeni fedha zake”,  ujumbe ambao umetafsiriwa kuwa huenda ni madeni anayowadai wasanii ndio imepelekea kuchukua maamuzi ya kutaka kuacha muziki.

Yogo anafahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kutayarisha midundo ya muziki wa bongo fleva ambapo mbali na kufanya kazi nyingi na AliKiba, amewahi pia kutayarisha midundo ya wakali kama The Mafik, Nedy Music, Nandy na wengine kibao

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke