You are currently viewing PRODYUZA WA MUZIKI NCHINI MAVO ON THE BEAT AMCHANA DJ PINYE KWA KUKOSOA MUZIKI WA GENGETONE

PRODYUZA WA MUZIKI NCHINI MAVO ON THE BEAT AMCHANA DJ PINYE KWA KUKOSOA MUZIKI WA GENGETONE

Prodyuza wa muziki nchini Mavo On The Beat DJ amemchana DJ mkongwe Pinye kwa kauli yake aliyotoa kuwa ni vigumu kupiga muziki wa Gengetone kwenye soko la Kimataifa kutokana na muziki huo kukosa ubora.

Akipiga stori na Plug TV prodyuza huyo amemsuta vikali DJ Pinye kwa kauli yake hiyo kwa kusema kuwa muda wake umepita na hana usemi kwenye  muziki wa Kenya hivyo aache swala la kuwaingilia wasanii wa Kenya ambao wanatia bidii kwenye kazi zao.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao wa kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na Mavo On The Beat ambapo wamemtaka  prodyuza ajikite kwenye ishu ya kuwashauri wasanii wa gengetone watoe muziki mzuri badala ya kuimba muziki ambao hauna mashiko kwa jamii.

Ikumbukwe juzi kati DJ Pinye kwenye mahojiano na Standard Media aliwapa wasanii wa Kenya changamoto kutoa nyimbo zenye ubora ambazo zitapigwa katika mataifa kama Nigeria, Afrika Kusini na mataifa mengine ambayo yanaongoza kimuziki duniani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke