You are currently viewing PRODYUZA WA NDOVU KUU AWASHAURI VIJANA KUWEKA AKIBA

PRODYUZA WA NDOVU KUU AWASHAURI VIJANA KUWEKA AKIBA

Msanii wa muziki nchini Krispar amewataka vijana kujenga tabia ya kuweka akiba kwa kuwa itawasaidia wakati wa matatizo.

Katika mahojiano yake na Kiss TV Krispar kuu amesema vijana wengi wamekuwa na mazoea ya kutumia pesa kwenye masuala ya starehe na anasa, jambo ambalo limepelekea baadhi yao kutotimiza malengo yao katika maisha.

Msaniii huyo amesema licha ya kwamba kuweka akiba ni ngumu kwa baadhi ya vijana ila wanapaswa kuwa na nidhamu kwenye matumizi ya pesa kuondoa gharama isioyokuwa na msingi.

Sanjari na hilo Hitmaker huyo wa ngoma ya “Ndovu Kuu” amewashauri wasanii kuwa na timu itakayowasaidia kusukuma muziki wao badala ya kuingia mikataba isiyoeleweka na lebo za muziki ambazo zinawafunga kisanaa.

Utakumbuka Krispar alipataa umaarufu nchini kipindi cha corona alipoachia wimbo wake uitwao ndovu kuu licha ya kuwa kwenye tasnia muziki kwa kipindi cha miaka 7.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke