Prodyuza mkongwe Washington juzi kati alizua mjadala mtandaoni alipoandika ujumbe wa kuwashinikiza baadhi ya wasanii nchini Uganda kumlipa mirahaba ya nyimbo alizofanya nao kipindi cha nyuma.
Ujumbe huo ulitafsiriwa na wengi kuwa huenda prodyuza huyo anapitia wakati mgumu kimaisha kutokana na kuyumba kiuchumi.
Sasa kwenye mahojiano yake hivi karibuni Washington ameibuka na kukanusha madai ya kufulia kiuchumi kwa kusema kwamba alikuwa anajaribu kuwakingia kifua maprodyuza wachanga ambao wananyanyaswa kwenye muziki wapate haki yao.
Kuhusu ishu ya wasanii kutomlipa pesa, Washington amesema waligharamia malipo ya huduma za studio ambayo ni tofauti kabisa na mirahaba ya nyimbo zao.