You are currently viewing PROMOTA ABTEX ATISHIA KUMALIZA CAREER YA PALLASO BAADA YA MSANII HUYO KUSUSIA PERFORMANCE YAKE

PROMOTA ABTEX ATISHIA KUMALIZA CAREER YA PALLASO BAADA YA MSANII HUYO KUSUSIA PERFORMANCE YAKE

Promota wa muziki nchini Uganda Abtex amesikitishwa na kitendo cha mwanamuziki Pallaso kutofika kwa wakati kwenye moja ya show aliyopewa nafasi kuperform huko Masaka.

Kwenye mkao na wanahabari Abtex amesema kitendo hicho sio cha kingwana na inaonesha ni jinsi gani pallaso hawashimu mashabiki zake ikizingatiwa kuwa walikuwa tayari wameshalipa pesa zao kwa ajili ya kumuona hitmaker huyo wa  ngoma ya “Malamu” akifanya performance yake.

Hata hivyo Abtex ametishia kuwashawishi mapromota wenzake nchini Uganda kususia kumpa pallaso shows kwenye matamasha yao ya muziki kwani msanii huyo anakwenda kinyume na mikataba yao maelewano.

Utakumbuka juzi kati pallaso alishinda kufika kwa wakati kwenye moja ya show huko masaka nchini uganda jambo ambalo lililazimu msanii huyo kupitia mitandao ya kijamii kuomba radhi kwa hatua yake hiyo baada ya mashabiki kuzua vurugu alipofika stejini kama amechelewa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke