You are currently viewing PROMOTA BALAAM BARUGAHARA AAPA KUWAPIGA MARUFUKU WASANII WANAOSUSIA SHOWS UGANDA

PROMOTA BALAAM BARUGAHARA AAPA KUWAPIGA MARUFUKU WASANII WANAOSUSIA SHOWS UGANDA

Promota wa muziki nchini Uganda Balaam Barugahara Atenyi ametishia kuwapiga marufuku wasanii wanaosusia shows licha ya kulipwa pesa zote kwa wakati.

Katika mkao na waandishi wa habari Jiji Kampala Balaam Barugahara amesema kamati ya waandaji wa maonesho ambayo inaongozwa na Promota Abtex ina mpango wa kuwapiga wasanii wa sampuli hiyo marufuku ya miaka 2 bila ya kuwapa mialiko kwenye matamasha yeyote ya muziki.

Kauli yake imekuja baada onesho lilofanyika huko Kyotera, Mukono nchini Uganda kukumbwa na vurugu ambayo ilisababisha uharibifu mkubwa wa mali ya mamilioni ya pesa.

Vurugu kwenye show hiyo ilitokea baada ya jenerata kuzima ghafla kutokana na ukosefu wa mafuta jambo ambalo lilipelekea waliokuwa wamehudhuria onesho hilo kukosa uvumili na kuzua rasbsha kufuatia waandaji wa show kuchukua muda mrefu kuwasha jenerata.

Lakini pia msanii Pallaso analaumiwa kwa kuchukua muda mrefu kujitayarisha ndani ya gari lake kabla ya kufika jukwaani kuwapa mashabiki burudani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke