You are currently viewing PROMOTA MUTIMA AMVUA NGUO SPICE DIANA KWA KUMVUNJIA HESHIMA

PROMOTA MUTIMA AMVUA NGUO SPICE DIANA KWA KUMVUNJIA HESHIMA

Siku chache baada ya Promota Robert Mutima kumuomba radhi msanii Spice Diana kwa kuchelewesha pesa zake, promota huyo ameibuka tena kumchana msanii huyo kwa kitendo cha kumuahibisha mbele ya mashabiki zake.

Mutima amesema alishangazwa na kitendo Spice Diana na huenda mrembo huyo anatumia mihadarati kabla ya kupanda jukwaani kwani njia ambayo alitumia kudai haki yake haikuwa nzuri.

Amesisitiza kuwa alikuwa ameshikika na majukumu mengine ambayo yalimkwamisha kutofika kwa wakati kwenye shoo hiyo kukamilisha malipo ya msanii Spice Diana.

Utakumbuka baada ya Spice Diana kusimamisha performance yake huko Masaka nchini Uganda alimtuhumu Mutima kwa kutokuwa mwazi kwenye ishu ya malipo ambapo alienda mbali zaidi na kuwataka mashabiki wabebe vifaa vyote vya kielektroniki kama njia ya kumuadhibu promota huyo jeuri.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke