You are currently viewing PROMOTA WA LONDON ATISHIA KUICHUKULIA HATUA KALI LEBO YA SWANGZ AVENUE

PROMOTA WA LONDON ATISHIA KUICHUKULIA HATUA KALI LEBO YA SWANGZ AVENUE

Promota wa Uganda wanayoishi mjini London Maama Africa ametishia kuhakikisha kuwa waimbaji wote wa Swangz Avenue wamepigwa marufuku kusafiri hadi London, lebo hiyo isipomlipa fidia ya euro 65000.

Promota hao anadai kuwa alilipa Euro 5000 ili Winnie Nwagi atumbuize London lakini siku ya tukio, Nwagi pamoja na Fik Fameika walikataa kutoa burudani kwa mashabiki hadi usiku wa manane wakati walipotumbuiza nyimbo chache.

Lakini pia wasanii hao walivunja mkataba na kutumbuiza kwenye shoo nyingine iliyopewa jina la “Chill and Grill” kwa kutumia kibali chake cha kazi, kitu ambacho anaona si cha kingwana.

“Nataka kuwafundisha uweledi waimbaji wa Uganda. Nililipa na kugharamia kila kitu kwa Winnie Nwagi, lakini alienda mbali zaidi na kutumbuiza katika hafla nyingine bila idhini yangu,” alisema katika mahojiano na MwanaYouTube.

Promota hao wameongeza, “Aliimba nyimbo chache tu baada ya kuchelewa kufika. Nimeiandikia Swangz avenue kuhusu kitendo hicho na ninatarajia jibu kabla ya Jumatatu la sivyo nitahakikisha kuwa wasanii wake wanapigwa marufuku kutumbuiza London.”

Hata hivyo Maama Africa wanahusisha kuporomoka kwa onyesho hilo na vitendo visivyo vya kitaaluma vya Winnie Nwagi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke