Rapa kutoka Marekani Pusha T hatimaye amefunguka sababu iliyomfanya kumaliza bifu yake na Drake ambayo ilidumu kwa miaka 10.
Kwenye mahojiano na Desus & Mero, Pusha T ameeleza kwamba, kuwa Baba mwaka 2020 ndio sababu pekee iliyomfanya aimalize bifu yake na Drizzy kwani kulimbadilisha mtazamo wake kwa ujumla hasa kuwahusisha watoto kwenye ugomvi.
Kama utakumbuka vyema, Pusha T ndiye aliifahamisha dunia kwamba Drake ana mtoto anaitwa Adonis lakini alimficha.
Kupitia freestyle yake ‘The Story of Adidon’ Pusha alichana “You are hiding a child, let that boy come home/ Deadbeat mothaf*cka, playin’ border patrol/ Adonis is your son.”
Hii ilimfanya Drake na baadaye kuthibitisha taarifa hizo kupitia album yake, Scorpion mwaka 2018.