You are currently viewing Q CHILLAH AMTUHUMU HARMONIZE KUWA MKABILA

Q CHILLAH AMTUHUMU HARMONIZE KUWA MKABILA

Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Q-Chillah amemtuhumu mwimbaji Harmonize kuwa na ukabila.

Kwenye mahojiano na kipindi cha “Interpol” Chillah amesema Harmonize amekuwa akiwapendelea sana wasanii wanaotoka kabila lake la Wamakonde kwenye shughuli zake za kimuziki huku akitaja sababu ya Country Wizzy kuondoka kwenye Label ya Konde Music Worldwide ilichangiwa na ukabila.

“Na ndio maana nilivyoondoka mimi sikuwa nimesainiwa, lakini Country Boy alikuwa amesainiwa lakini alishindwa kukaa na kuvumilia. Ana ukabila kidogo ambao sio mzuri, ambao Diamond Platnumz hana huo ukabila wala AliKiba hana huo ukabila, inabidi autoe.” Amesema Q Chillah.

Utakumbuka Q Chief mwaka wa 2019 alifanya kazi na Harmonize ambapo walitoa Return of Q Chillah EP yenye jumla ya nyimbo 3 za moto.

Hata hivyo walikuja wakaacha kufanya kazi pamoja walipoingia kwenye ugomvi baada ya Harmonize kumnyang’anya zawadi ya gari aliyompa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke