Marapa Queen Latifah na Ludacris kutoka Marekani wataonekana kwenye filamu mpya ya Netflix “End Of The Road” ambayo itaachiwa rasmi September 9, mwaka wa 2022.
Filamu hiyo itagusa maisha ya mjane mmoja (Brenda) ambaye ndiye Queen Latifah, baada ya kufutwa kazi akaamua kuichukua familia yake na kuondoka kwa ajili ya kuanza maisha mapya.
Wakati wapo safarini (Road Trip), walisimamishwa katikati ya Jangwa, New Mexico bila msaada wowote. Muuaji hatari alianza kuwafuatilia. Brenda na familia wanatakiwa kujifunza kupambana ili kuweza kujiokoa kwenye sekeseke hilo