Mwimbaji mkongwe wa Muziki wa R&B Robert Sylvester Kelly (R Kelly) amekutwa tena na hatia ya makosa 6 kati ya 13 katika kesi zinamkabili ikiwemo kujihusisha na picha za ngono za watoto wadogo.
Mwimbaji huyo alishtakiwa katika mji aliozaliwa wa Chicago kwa mashtaka 13 ikiwa ni pamoja na kutengeneza picha za unyanyasaji wa watoto, kuwashawishi watoto kufanya ngono, yaliyofanyika 2008.
Kelly amekutwa na hatia ya makosa hayo katika mahakama ya mjini Chicago Jumanne ya wiki hii. Inaelezwa endapo kukiwa na hukumu juu ya mashtaka hayo sita, adhabu yake huenda ikaanza na miaka 10 hadi 90 jela.
Ikumbukwe kwamba kwa sasa R Kelly anatumikia kifungo cha miaka 30 baada ya hukumu yake Juni 29, kwa makosa ya kingono na ulaghai.