Mwimbaji Robert Kelly maarufu R.Kelly ambaye kwa sasa anatumikia miaka 30 ya kifungo chake gerezani, amekanusha taarifa ya mrembo Joycelyn Savage ambaye ni mhanga katika makosa yake, kudai ana ujauzito wake.
Mwanasheria wa Kelly, Jennifer Bonjean ameiambia TMZ hamna ukweli wowote juu ya hilo.
Mrembo Joycelyn Savage kupitia chapisho ndani ya kitabu chake kipya kilichotoka Ijumaa ya wiki iliyopita, alitoa taarifa ya kuwa na ujauzito wa Kelly licha ya kutoeleza ni namna gani alipata ujauzito huo, hali ya kuwa R.Kelly amekuwa kwenye mikono ya sheria tangu Julai, mwaka 2019.
Aidha, kwenye chapisho la mrembo Joycelyn Savage alieleza kwamba R.Kelly alifurahishwa na taarifa hizo za ujauzito wake