Mwanamuziki kutoka Marekani R. Kelly kuanza kupandishwa tena kizimbani, shtaka lake la mwaka 2008 ambalo anakabiliwa nalo kwa kujihusisha na masuala ya kutengeneza maudhui ya ngono kwa watoto (Child Pornography) limeanza kusikilizwa Jumatano.
Taarifa kubwa ni kwamba Wazee wa Baraza la Mahakama wameruhusiwa kutazama mikanda mitatu ya ngono ambayo Mwanamuziki R. Kelly alikuwa akijirekodi na mabinti hao wadogo kama ushahidi mbele ya Mahakama.
Mbali na msumari huo, binti mmoja ambaye jina lake limefichwa, naye ameapa kutoa ushahidi kuwa alifanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kingono huku akirekodiwa na R. Kelly alipokuwa na umri wa miaka 14. Video yake pia itaoneshwa mbele ya wazee wa baraza la Mahakama ili kumtambua R. Kelly ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 30 Jela