You are currently viewing RABADABA AFUNGUKA KUHUSU GHARAMA YA KUANDAA VIDEO ZA MUZIKI UGANDA

RABADABA AFUNGUKA KUHUSU GHARAMA YA KUANDAA VIDEO ZA MUZIKI UGANDA

Mwanamuziki wa Dancehall kutoka nchini Uganda Rabadaba anasema gharama ya kuaandaa video nchini Uingereza ni nafuu sana ikilinganishwa na Uganda.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Rabadaba Anasema waongozaji wa video nchini Uganda wanatoza wasanii pesa nyingi lakini wanashindwa kutayarisha video zenye ubora.

“Utayarishaji wa video ni wa bei nafuu zaidi London ikilinganishwa na Uganda. Huko nyumbani, wakurugenzi wanadai pesa nyingi lakini wanazalisha kazi duni. Hapa London, kazi bora hutolewa kwa bei nafuu,” anaelezea katika mahojiano.

Rabadaba amekuwa akiishi London kwa zaidi ya mwaka mmoja na juzi kati aliachia video mpya ya wimbo wake uoitwa “Ffe Banene” ambayo ilitayarishwa na kuelekezwa jijini London.

Rabadaba alipata umaarufu mwaka wa 2009 baada ya kuachia wimbo wake uitwao ‘Bwekiri’. Na Ability akishirikiana na wasanii wa Goodlyfe.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke