You are currently viewing Ragga Dee afunguka kustaafu muziki

Ragga Dee afunguka kustaafu muziki

Msanii mkongwe kwenye muziki kutoka nchini Uganda Ragga Dee amedai kuwa hana mpango wa kustaafu muziki hivi karibuni licha ya kuwa hajakuwa akiachia nyimbo katika miaka ya hivi karibuni.

Kwenye mahojiano yake na kituo kimoja cha redio nchini uganda Ragga Dee amethibitisha kuwa ataendelea kufanya muziki hadi atakapopumua hewa yake ya mwisho duniani.

“Muziki ipo ndani mwangu. Nimekuwa nikifanya tangu utotoni. Siwezi kuacha muziki kamwe. Ragga Dee alieleza.

Ragga dee ni moja kati ya wasanii walioacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini uganda na alipata umaarufu zaidi Afrika Mashariki kupitia wimbo wake uitwao “Ndigida.”

Mwaka wa 2016 aligeukia siasa kwa kuwania kiti cha umeya wa jiji la kampala kwenye uchaguzi mkuu lakini kwa bahati mbaya alishindwa na Erias Lukwago.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke