Lejendari wa muziki kutoka nchini Uganda Ragga Dee amejitenga na madai ya kufuja pesa za madeejay alizopewa na Gen. Salim Saleh.
Hitmaker huyo wa “Letter O” amekanusha tuhuma hizo ambazo ziliibuliwa dhidi yake na Madeejay nchini Uganda wakisema kwamba alikimbia na pesa zao ambazo walipewa na serikali kutokana na makali ya corona.
Akiwa kwenye mahojiano na runinga moja nchini Uganda Ragga Dee amesema aliupokeza muungano wa madeejay nchini humo shillingi milloni 10 na ilipokelewa DJ Nimrod.
Mwanamuziki huyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa tamaa imewaponza madeejay wa uganda kwani wengi wao wanajidhalalisha kwa kuanika shida zao mitandaoni.
Hata hivyo amedai kuwa aliwahi kuwa deejay kipindi cha nyuma na anafahamu kila kitu kuhusu hu-deejay, hivyo amewataka madeejay wa uganda kukoma kujiona wa maana kuliko watu wengine