Msaniii mkongwe kwenye muziki nchini uganda Ragga Dee amekuwa sehemu ya tasnia ya muziki nchini Uganda tangu miaka ya 1990.
Juzi kati, amekuwa akichukua nafasi za uongozi kwa nia ya kusaidia wanamuziki wenzake.
Good news ni kwamba amechaguliwa kuwa mjumbe wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi (PSFU) ambapo atakuwa akiwakilisha Tasnia ya Sanaa, Utamaduni na Ubunifu.
Tangazo hilo limetolewa na idara ya mawasiliano ya PSFU kupitia mitandao yao ya kijamii.
“Tunamkaribisha rasmi Daniel Kazibwe almaarufu Ragga Dee kama Mjumbe wa Bodi ya PSFU anayewakilisha Tasnia ya Sanaa, Utamaduni na Ubunifu,” tangazo hilo lilisomeka.
Akizungumzia baada ya uteuzi huo, Ragga Dee amesema atatumia ushawishi wake kwenye muziki kuunganisha tasnia ya burudani nchini Uganda.