Msanii mkongwe kutoka Uganda Ragga Dee amezikingia kifua tuzo za Janzi Awards akisema tuzo hizo ni tofauti na tuzo ambazo tayari zimeandaliwa nchini Uganda.
Tuzo hizo ambazo ziliandaliwa wiki hii iliyopita imekosolewa na baadhi ya wasanii kwa kukosa uwazi.
Ragga dee amesema tuzo za Janzi zina dhamana kubwa ya takriban shillingi 112,998.26 za Kenya, hivyo mtu anaweza iuza na akapata pesa ambazo zimtasaidia kimaisha.
Hitmaker huyo wa “Ndingida” amekanusha uvumi unaotembea mitandaoni kuwa kamati ya tuzo hizo ilipewa takriban shillingi millioni 28.6 kuandaa hafla hiyo kwa siku mbili akishangaa ni wapi walipata pesa hizo.
Hata hivyo amedokeza kuwa watu ambao wamekuwa wakitoa lalama juu ya tuzo hizo ni wale ambao hawakushinda tuzo hata moja.