Mwanamuziki anayekuja kwa kasi nchini Uganda Rahmah Pinky amevunja kimya chake juu ya kutengana na meneja wa vipaji, Jeff Kiwa.
Pinky ameelezea kuwa Jeff Kiwa alipoteza mweelekeo kwenye suala la kusimamia muziki wake na akaanza kumtaka kimapenzi, jambo ambalo anadai hakuweza kulivumilia.
“Mawazo yake yalibadilika na akaanza kutaka mambo mengine kutoka kwangu, ilibidi niikimbie lebo yake ya TNS kwa sababu sikutaka kukubali njia aliyotaka niifuate,” alisema katika mahojiano na runinga moja nchini Uganda.
Kauli ya Pinky imekuja mara ya kudaiwa kuwa alitimuliwa kwenye lebo TNS inayoongozwa na Jeff Kiwa kwa kukosa nidhamu.
Inaidaiwa kuwa licha ya kuonywa mara kwa mara kubadili mienendo yake, alipuuza ushauri wa uongozi wake na kuendelea kuvuta shisha huku akitoka kimapenzi na wanaume tofauti kwenye nyumba ambayo lebo ilimkodishia kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake za kisanaa.