Kocha wa Manchester United Ralf Rangnick ameeleza kuwa hatalazimika kumshawishi kiungo wake, Paul Pogba kuondoka ndani ya klabu hiyo ikiwa mchezaji huyo atataka kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Pogba alirejea England akitokea Dubai, mwishoni mwa juma lilopita baada ya kuwa kwenye matibabu kwa muda wa wiki tatu lakini Rangnick ametoa muongozo kuwa wachezaji wanatakiwa kutibiwa katika kambi ya timu hiyo, Carrington pindi wanapoumia.
“Wachezaji wanatakiwa kuwa na nia ya kuichezea klabu na kubaki katika klabu kubwa kama Manchester United.
“Kama kuna mchezaji anataka kuondoka na hataki kuichezea Manchester United sidhani kama ni sahihi kumshawishi aendelee kubaki,” amesema Rangnick.