Rapa kutoka Marekani Cardi B amefunguka wazi kuwa amechoka kuwa maarufu, hii ni baada ya kumalizika kwa onesho la Met Gala 2022 Jijini New York Jumatatu wiki hii.
Cardi B ameutumia ukurasa wake wa Instagram kwenda live na kusema kwamba umaarufu si kitu kizuri kwa upande wake huku kuwataka watu wasitamani umaarufu bali watamani kuwa matajiri.
“Ninauchukia umaarufu, nachukia kuwa maarufu. Nachukia sana. Acha niwaambie kitu kimoja, kama umewahi kutamani kuwa tajiri na maarufu, usitamani kuwa maarufu, tamani kuwa tajiri.” Amesikika akiwa Instagram live.
Hii sio mara ya kwanza kwa Cardi B kuonesha hautaki umaarufu, aliwahi kuufuta ukurasa wake wa Twitter kwa kueleza tatizo hilo.